Ubaguzi ni jambo la msingi na lenye nguvu katika kufanya maamuzi kuhusu mambo ya kiafya. Ubaguzi kulingana na uraia, kabila, rangi ya ngozi, tabaka, dini, uenyeji au uhamiaji huathiri afya ya watu binafsi na jamii ulimwenguni kote. Lengo letu ni kupunguza athari mbaya za ubaguzi ambazo husababisha afya duni. Uraia na Afya ni mkusanyiko wa wasomi, wasanii, wakereketwa na wanaharakati, watengenezaji sera, mashirika ya kijamii na watu binafsi. Hiki kitakuwa ni kitovu cha kuchunguza jinsi ubaguzi wa rangi huathiri afya na mikakati ya kuboresha afya. Tunachochea ili kupata usawa wa kiafya kwa wote. Njoo uungane nasi.

Race & Health Quarterly

Our new quarterly newsletter.